Mwanamke wa Ikonda Makete Avamiwa Usiku na kujeruhiwa kisa Wivu wa Kimapenzi (Audio)

Viongozi wilayani Makete mkoani Njombe wameaswa kutoa ushirikiano pindi matukio Ya kihalifu yanapotokea katika maeneo yao ili kuwatumikia wananchi wanaowaongoza.

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kitongoji cha Ikonda bondeni Kata ya Tandala wilayani Makete Bi Roida Ilomo alipokuwa akitolea ufafanuzi wa tukio la mwananakitogoji wake aitwaye Anna Mahenge kuvamiwa usiku nyumbani kwake na mkazi wa kitongoji cha Singida aitwaye Happy Mgaya



Bi Roida amesema usiku wa tarehe 21 Mei mwaka huu alisikia yowe zikipigwa nyumbani kwa mtuhumiwa hali iliyomlazimu kwenda nyumbani kwa Bi. Anna Mahenge kujua kulikoni na kubaini kuvamiwa kwa mkazi huyo ambaye amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake

Kutokana na kijiji kukosa sehemu ya kumhifadhi mtuhumiwa usiku huo walilazimika kumpeleka kwa mwenyekiti wa kitongoji cha Singida kijiji cha Tandala Bw Christopha Sanga kumuhifadhi mtuhumiwa ili asubuhi afikishwe kwenye vyombo vya sheria ambaye kwa sasa anatuhumiwa kumtorosha mtuhumiwa huyo.

Mwandishi wa blog hii amezungumza kwa njia ya simu na Afisa mtendaji wa kijiji cha Tandala Bw Ambele Sanga kuhusiana na tukio hilo ambapo pamoja na mambo mengine amekanusha taarifa kuwa alipigiwa simu kuhusu kumuhifadhi mtuhumiwa na badala yake amesema aliwapa ushauri kuwa wamuhifadhi mhuhumiwa huyo hadi asubuhi ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria kwa kuwa yeye alikuwa Makete mjini kwenye matibabu

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Singida Bw. Christopha Sanga amekana tuhuma za kuhusika kumtorosha mtuhumiwa huku akikiri kitendo cha mtuhumiwa kutoroka na kwenda kusikojulikana akiwa nyumbani kwake.

Naye anayedaiwa kufanyiwa tukio hilo Bi Anna Mahenge amekiri kufanyiwa tukio hilo majira ya saa tano za usiku.

Mtuhumiwa wa tukio hilo ambaye ni mkazi wa kitongoji cha Singida kijiji cha Tandala kata ya Tandala wilayani Makete amekimbilia kusikojulikana na suala hilo tayari limeripotiwa kwa jeshi la polisi kwa hatua zaidi za kisheria


Na Asukile Mwalwembe


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo