"Mgomo" wa baadhi ya Wafanyabiashara Tandala Makete (Audio)

Wafanyabiashara wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kufuata magizo yatolewayo na serikali kuhusu maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuuzia mazao yao.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Tandala wilayani hapa walipokuwa wakizungumzia suala la baadhi ya wafanyabiashara wadogowadogo kuuzia mazao yao eneo la stendi ya zamani Tandala jirani na kituo cha bodaboda badala ya stendi mpya iliyopo kitongoji cha Singida.

Wananchi hao wameongeza kuwa serikali inatakiwa kupiga marufuku magari yote yanayo simama eneo hilo la stendi ya zamani ili kwenda kusimama stendi mpya kama wanataka kudhibiti wafanyabiashara hao.

Kwa upande wao wafanyabiashara hao wameelezea sababu zinazo wafanyebiashara eneo hilo kuwa ni kutokana na wanunuzi hawaendi stendi mpya hivyo kulazimika kuwafuta stendi ya zamani ambapo kuna wateja wengi.

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Tandala Bw, Andowisye Memba amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo huku akisema wao kama viongozi wana mpango wa kuhamasisha wakulima na watu wengine wasio na maeneo maalum ya kufanyia biashara kwenda kuuzia bidhaa zao stendi ya mpya ya Singida

Kupata sauti Bonyeza hapa:-


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo