Mkazi wa Kitongoji cha Majengo Kata ya Kabarimu Wilaya ya Bunda Mjini mkoani Mara anashikiliwa na polisi kwa
tuhuma za kumchapa mtoto wake Wakuru Rungu (9), viboko
viwili kichwani na kumsababisha kifo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhan Ng’anzi
amesema tukio hilo lilitokea Mei 15 saa kumi na moja jioni
baada ya mama huyo kumtuhumu mwanaye kuiba Sh8,000.
Kamanda Ng’anzi amesema mtoto huyo ni mwanafunzi wa
darasa la pili katika Shule ya Msingi Kabarimu.
“Alimpiga sehemu ya kisogo hivyo kusababisha kupoteza mwelekeo,” alisema Ng’anzi.
