Wananchi wa kata ya Tandala wilayani Makete mkoani Njombe wameshauriwa kutunza miundombinu ya barabara.Kauli hiyo imetolewa hii leo na diwani wa kata ya Tandala ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh, Egnatio Mtawa wakati wa zoezi la Kutengeneza barabara ya kuanzia njia panda Ya Usagatikwa hadi kijiji cha Usagatikwa ambapo diwani Mtawa amewaomba wananchi baada ya zoezi hilo la kufungua mifereji ya maji.
Pia Mtawa ameelezea zoezi zima la UKARABATI wa barabara za kata ya Tandala huku akisema kuwa zoezi hilo litasimama Kwa muda kutokana na greda kwenda kufanya kazi ya mkandarasi kwa ajili ya maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru.
Kwa upande wake mtendaji wa kata ya Tandala Bi, Karmela Malley ameeleza kuridhishwa na zoezi hilo katika kata yake.
Aidha wananchi wa kata ya Tandala nao wakaelezea zoezi hilo huku wakisema Litasaidia uwezekano wa kupitisha kiurahisi mazao yao na kuwasihi wananchi wengine kutunza miundombinu hiyo.
Na Asukile Mwalwembe