Zaidi ya watu 40 wanusurika kifo katika ajili mkoani Mwanza

Zaidi ya watu 40 wamenusulika kifo kati yao 15 wamejeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka katikati ya jiji la Mwanza kwenda Igombe kuacha njia na kutumbukia kwenye mtaro wa barabara ya Pasiansi Airpoti eneo la iloganzala hali iliyosababisha msongamano wa magari katikati ya jiji.

Aliyekatika mkono kutokana na ajali ya gari la abiria namba T 764 AMD aina ya Isuzu na baadhi ya majeruhi waliofikishwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Mwanza Sekou Toure wakibainisha chanzo cha ajali hiyo.
 
Akithibitisha kupokea majeruhi 12 afisa muuguzi katika hospitali ya rufaa mkoa wa Mwanza Sekou Toure Bi.Leya Mwalongo amesema kuwa kati ya majeruhi 12 mmoja hali yake siyo nzuri atahamishiwa hospitali ya rufaa bugando.
 
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza ACP Japhet Lusingu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyosababisha majeruhi 15 ambapo dereva wa gari hilo ametoroka na kwamba juhudi za kumtafuta zinaendelea.     


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo