Waziri Mkuu atoa agizo zito kwa maafisa biashara wote Nchini

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza maofisa biashara wa wilaya, mikoa na Taifa kukagua maghala yote ya wafanyabiashara walioficha sukari na kuwachukulia hatua.

Waziri Majaliwa alisema hayo leo asubuhi wakati akihitimisha mjadala wa hotuba ya mapato na matumizi ya ofisi yake na kuliomba Bunge likubali kupitisha.

Waziri Mkuu alisema ni kweli kwamba kuna upungufu wa sukari nchini, ingawa pia upo udanganyifu kwa baadhi ya wafanyabiashara.

Alisema takwimu kutoka kwa wataalamu zinaeleza kwamba mpaka sasa kuna tani 37,000 za sukari katika maghala nchini, lakini imekuwa haionekani kwa sababu wafanyabiashara wakubwa wameificha ili waiuze kwa bei kubwa.

“Ninawaagiza maafisa wa biashara kushughulikia suala hili, na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuwa wamekwenda kinyume na taratibu  tulizojiwekea,”  alisema Majaliwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo