Baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kuondoa shitaka la utakatishaji fedha katika kesi inayowakabili Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni, upande wa mashitaka umekata rufaa ya kupinga mwelekeo wa kuondolewa kwa shitaka hilo, anaandika Faki Sosi.
Kitillya,
alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu
wa Idara ya Ushirikiano na Uwezekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi
Solomoni, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic.
Amilis
Mchaura, Hakimu Mkazi Kisutu amesema kuwa, shitaka la nane
linalowakabili watuhumiwa hao lina upungufu kisheria hivyo mahakama
italifuta shitaka hilo.
Jopo
la mawakili wa upande wa utetezi linaongozwa na Dk. Lingo Tenga
liliomba mahakama kuwapa wateja wao dhamana yenye masharti nafuu.
Baada
ya Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi kusimamisha kusikiliza kesi hiyo kwa
dakika 30, aliporejea tu, Oswadi Tibabyekonya, Mwanasheria Mwandamizi wa
Serikali alileta notisi ya rufaa kutoka Mahakama Kuu iliyokuwa ikipinga
mwelekeo wa kufutwa kwa shitaka la utakatishaji fedha.
Hakimu Mchaura baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, alihailisha shauri hilo na kwamba, uamuzi atautoa tarehe 29 Aprili mwaka huu. Watuhumiwa wote wamekosa dhamana wamerudishwa rumande.
