Hivi karibuni Halmashauri ya wilaya ya Makete ilipiga marufuku vijana waliokuwa wakifanya kazi ya kuosha vyombo vya usafiri ikiwemo magari na pikipiki katika mto uliopo karibu na ukumbi wa MTC Tandala Makete Njombe
Lengo la kutolewa katazo hilo ni kunusuru uharibifu wa mazingira unaotokana na uoshaji huo wa magari na pikipiki lakini pia na utekelezaji wa sheria za mazingira zinavyotaka kuwa shughuli zozote zisifanyike kwenye mito na vyazo va maji ndani ya mita sitini
Eddy Blog imetembelea eneo hilo siku nne sasa baada ya amri hiyo kutolewa, tumeshuhudia vijana wametii agizo hilo na sehemu hio ipo salama kwa kuwa hakuna kazi za uoshaji magari na pikipiki zinazoendelea, hapa nimekuwekea picha kadhaa ziangalie
Muonekano wa Mto huo
Bomba lililokuwa likitumiwa na vijana hao Muonekano wa eneo hilo kwa sasa Chupa za maji zikiwa katika mto huo
Takataka katika eneo hilo Kibao cha katazo kilichowekwa na wataalamu wa mazingira