skip to main |
skip to sidebar
Nyumbani kwa Papa Wemba ni Vilio Tu, Angalia Picha hizi
Punde baada ya kupokea habari ya kifo cha ghafla cha gwiji wa muziki wa
Soukus Papa Wemba akiwa katika tamasha la muziki la Abidjan Ivory Coast
, maelfu ya jamaa marafiki na mashabiki wake walianza kumiminika
nyumbani kwake huko Kinshasa katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Dadake Akita Helena na mamake Papa Wemba wamekuwa wakiwapokea waombolezaji nyumbani kwao Matonge.
Nyota wa muziki wa Soukous ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo- Papa Wemba alifariki dunia baada ya kuzirai jukwaani

Papa Wemba ambaye jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene
Kikumba, alianguka na kufa jukwaani akiwatumbuiza maelfu kwa maelfu ya
mashabiki wake waliojitokeza katika tamasha la muziki mjini Abidjan
Ivory Coast.
Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.

Msanii huyo nguli mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni anasemekana
alianza kutetemeka, kisha akaanguka na kuzirai, alipokuwa akitumbuiza
jukwaani Abidjan.
Papa Wemba, kama alivyofahamika na mashabiki wake, alikuwa na umri wa miaka 66 na alikuwa amepata uraia wa Ubelgiji.
Vibao vyake ni kama Mwasi,show me the way, Yolele,
Mama,Proclamation"Chouchouna" (Papa Wemba), "Eluzam" na " Mbeya Mbeya"
(Evoloko Lay Lay), "BP ya Munu" (Efonge Gina), "Mwana Wabi" , "Mizou"
(Bimi Ombale) , "Zania" (Mavuela Somo.
Chanzo:BBC
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi