Msafara wa Waziri wapotea ukienda shuleni

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiwa katika ziara ya kutembelea shule ya msingi Nzuguni B. Kulia kwake ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Mstahiki Jaffari Mwanyemba aliyeongozana na Mhe. Naibu waziri katika ziara hiyo.
msafara wa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman
Jafo leo asubuhi ulipotea njia kutokana na watumishi wa Manispaa ya
Dodoma kutojua eneo ambalo waziri huyo alikuwa analitembelea.

Waziri Jafo alikuwa amepanga kufanya ziara kwenye Shule ya Msingi ya
Nzuguni B kwa lengo la kuangalia mapungufu, hasa tatizo la uhaba wa
madawati, lakini hakufika kama alivyotarajia kutokana na watumishi hao
kutojua eneo ambalo shule hiyo iko.

Shule hiyo haijawahi kutembelewa na ofisa elimu tangu mwaka 2007 licha
ya kuwa kilomita 6 kutoka katikati ya mji.

Naibu Waziri alikasirishwa na kitendo hicho akawataka watumishi wa idara
ya Elimu wajipime kama wanastahili kuendelea kufanya kazi.

“Mstahiki Meya, mimi niliona wazi kuwa watumishi wako wananipoteza,"
alisema Waziri Jafo.

"Nimechukia sana na hawa watu. Tatizo lao ni kwamba hawajawahi kuja
katika shule hii tangu mwaka 2007, lakini wamekaa ofisini tu.
Ikiwezekana waondolewe na kupelekwa vijijini,” alisema Jafo.
 
lakini baadae alifika shuleni hapo,

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa na utaratibu wa kutembelea maeneo yao ya kazi mara kwa mara ili kujionea hali halisi na kutatua kero zilizopo.

Akizungumza na walimu wa shule ya msingi Nzuguni B. wakati wa ziara aliyoifanya kutembelea shule  hiyo na shule ya sekondari Nzuguni A., Mhe. Jafo alisema watumishi hawawezi kufanya kazi kwa ubora iwapo watakuwa hawatembelei na kukagua maeneo yao ya kazi.

“ Kumekuwa na uzembe kwa Wakuu wa Idara kutokusikiliza matatizo ya chini, kutowatembelea watumishi waliopo chini yetu inawasababishia kukosa mahali pa kusemea shida zao na kuchanganyikiwa. Ni vizuri kuwa na  utaratibu wa kuwatembelea watumishi tunaowaongoza ili kujua shida zao na kuzitatua. Alisisitiza Mhe. Jafo.

Aidha, aliwataka walimu wa shule za msingi Nzuguni B na Shule ya sekondari Nzuguni A kuweka utaratibu wa kuweka malengo na kujipima kuona walichokifanya ili kupata matokeo tarajiwa.

Wakati huo huo, Naibu  Waziri wa Nchi Jafo ametoa Mabati 164 ili kuchangia  ujenzi wa Madarasa ya shule ya msingi Nzuguni B iliyopo kata ya Nzuguni katika halmashauri ya Mji wa Dodoma.

Mhe. Jafo alitoa Mabati hayo baada ya kufanya ziara ya kutembelea shule hiyo ili kujionea hali halisi ya maendeleo yake ikiwa ni moja ya taratibu alizojiwekea za kutembelea maeneo mbalimbali yanayohudumiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI ili kujionea changamoto mbalimbali zilizopo katika utoaji  wa huduma na kuzitafutia ufumbuzi.

Katika ziara hiyo Mhe. Jafo alikuta Idadi  kubwa ya watoto walioandikishwa  kujiunga na darasa la kwanza hali iliyopelekea kukosekana kwa vyumba vya  kutosha kwa ajili ya kujifunzia wanafunzi ambapo kwa kutatua kero hiyo, shule hiyo imeanza ujenzi wa vyumba vya madarasa na kwa upande wake alichangia bati 164 ili kuwezesha madarasa hayo kukamilika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo