Mwenyekiti
wa UVCCM Mkoa wa Arusha Lengay Ole Sabaya akitoa tamko kwa waandishi wa
habari jana jijini Arusha,ambapo amemtaja Mathias Manga na washirika
wake kuwa ni tatizo kubwa ndani ya chama na kwamba kama akiendelea
kuwepo ni Dhahiri kuwa anaweza kukisambaratisha chama hicho kutokana na
kugawa makundi kwa vijana wa chama hicho kutokana na fedha zake.(Habari
Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Katibu hamasa Mkoa wa Arusha Lucas Msomi akisisitiza jambo katika kikao na waandishi wa habari
Baraza
la vijana mkoa wa Arusha la chama cha mapinduzi uvccm limetangaza
kumvua ukamanda wa vijana wilaya ya Arumeru bw,Mathias Manga kutokana na
kukiujumu chama kwa muda mrefu hali ambayo imekuwa ikididimiza jitihada
za kurejesha imani ya chama hicho.
Bw,Manga
ambaye ni mafanyabiashara maarufu wa madini Mkoani Arusha amekuwa
akituhumiwa kwa muda mrefu kuwa namhausiano ya karibu ya aliyekuwa
mgombea urais kwa tiketi ya Ukawa Edward Lowassa na kusahau kufanya
majukumu ya kichama ambayo yamempa uongozi wa Ukamanda wa vijana wilaya.
Akitoa
maelezo ya tamko hilo mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha Lengay Ole
Sabaya amemtaja Mathias Manga na washirika wake kuwa ni tatizo kubwa
ndani ya chama na kwamba kama akiendelea kuwepo ni Dhahiri kuwa anaweza
kukisambaratisha chama hicho kutokana na kugawa makundi kwa vijana wa
chama hicho kutokana na fedha zake.
Aliongeza
kuwa kutokana na kumvua ukamanda kamanda huyo UVCCM Mkoani hapa
haitakuwa tayari kushiriki kikao chochote cha kamati ya siasa ambapo
Manga atashiriki kama mjumbe katika kikao hicho.
,,Sitashiriki
kwa namna yeyote na vijana wangu kwenye kikao cha kamati ya siasa Mkoa
ama kikao kingine ambacho kitanikutanisha na Mathias Manga na nawataka
wanachama wa chama cha mapinduzi kuona kama ni halali kwa huyu aliyeitwa
kamanda wa vijana kuendelea kushikilia kadi yao,,Alisema Ole Sabaya
Akitoa
onyo kwa makamanda wilaya ya Arusha mjini,Longido na Monduli kujipima
na kujitathimini kabla ya kufikia uamuzi kama bado wanafaa kuendelea na
hadhi ya ukamanda wa wilaya ama laa,na wakijiona hawatoshi tunawashauri
wakae pembeni mapema kabla ya kutumbuliwa jipu.
Baraza
linakiomba chama cha Mapinduzi kupitia tathini ya uchaguzi mkuu wa
mwaka jana wale wote walioshiriki kukihujumu chama kuanzia ngazi ya
matawi,kata,wilaya na Mkoa washughulikiwe kwa mujibu wa taratibu za
kimaadili kabla ya uchaguzi wa chama 2017 vinginevyo wakiachwa
watashiriki tena kufanya uhasi dhidi ya chama sanjari na kupandikiza
mamluki.
Hata
hivyo mwenyekiti huyo ametengua uteuzi wa wajumbe watano wa baraza
katika nafasi za kuteuliwa ilidumu toka mwaka 2012 na kuunda kamati mpya
chini ya mwenyekiti Lengai Ole Sabaya huku akiwataka viongozi wa chama
hicho kumuunga mkono Rais JohnPombe Magufuli kwa jitihada zake za
kupeperusha bendera ya chama na kufanya kazi kwa uadilifu na kubeba
kauli ya HAPA KAZI TU.