Waziri Maghembe atumbua jipu la nyani wekundu 61 waliokuwa wakiibwa

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof JUMANNE MAGHEMBE amewasimamisha kazi baadhi ya watendaji wakuu wa Wakala wa huduma za Misitu-TFS na mameneja saba wa kanda wa wakala huo pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa wanyama pori Dk Charles Mulokozi kutokana na makosa mbalimbali yaliyoisababishia hasara serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Waziri Maghembe amesema wakala wa Misitu Tanzania watendaji wake wameshindwa kusimamia ipasavyo rasilimali za mazao ya misitu, na kusababisha uvunaji holela na kupelekea kuchomwa moto kwa magogo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milion 500 ambayo yalitaifishwa na serikali baada kubainika kuvunwa bila vibali.
Magogo hayo yaliyokamatwa wilayani Kalambo Mkoa wa Rukwa, yalitakiwa kukusanywa na kupelekwa kwenye ofisi ya Mkuu wa wilaya, lakini TFS walishindwa kusimamia ukusanyaji wake na hatimaye kuchomwa moto na watu wasiojulikana.
Katika hatua nyingine Waziri wa Maliasili na Utalii amemsimamisha kazi  Dk. Charles Mulokozi ambaye alikuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori baada ya kubainika kutoa vibali vya kusafirisha nyani 61 licha ya kwamba alikataliwa kutoa vibali hivyo.
Kwa mujibu wa Prof Maghembe alipata taarifa za kundi la watu ambalo lilikuwa likikusanya nyani kutoka mapori na hifadhi mbalimbali ambapo nyani 450 walibainika kukusanywa na hivyo kuamua kuzuia vibali vyote vya kusafirisha wanyama lakini Dk Mulokozi aliamua kutoa kibali cha kusafirisha nyani hao kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro.
Akitangaza hatua zilizochukuliwa dhidi ya nyani hao ambao walikuwa wakisafirishwa kwenda nchi za Ulaya Mashariki,


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo