Baada ya kuzagaa taarifa katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Makete mkoani Njombe kuwa mbunge wa jimbo hilo Prof. Norman Sigalla King amefukuzwa bungeni, hatimaye mbunge huyo amezungumzia tuhuma hizo
Prof. Sigalla ambaye ni mbunge wa jimbo la Makete kupitia Chama cha Mapinduzi CCM kwa kipindi cha miaka mitano (2015-2010) amesema hakuna ukweli wowte kuwa amefukuzwa kushiriki vikao vya bunge na kuongeza kuwa mbali na hilo hakuna mbunge hata mmoja wa CCM ambaye amefukuzwa bungeni
"Ndugu mwandishi mimi nakuthibitishia hili, kuwa hizo taarifa ni za uongo na uzushi mkubwa, mimi sijawahi kufukuzwa bungeni na wala haitakaa itokee, labda nifukuzwe wakati nikitetea wananchi wangu wapate barabara ya lami ya Njombe Makete Mbeya lakini si vinginevyo" amesema Mbunge huyo
Aidha ameliomba jeshi la polisi kuingilia kati suala hilo na kumsaka mtu ama watu ambao wamevumisha taarifa hizo ambazo hazina ukweli wowote kwa kuwa wao wana uwezo mkubwa wa kufanya hivyo na kuongeza kuwa sasa sio muda wa majungu badala yake uchaguzi umekwisha na yeye ndio mbunge hivyo kilichobaki ni kufanya kazi aliyotumwa na wananchi wa jimbo la Makete