Kauli ya kwanza ya Mbunge Halima Mdee baada ya kutoka Rumande

HALIMA Mdee, Mbunge wa Kawe amesema, hekaheka zinazofanywa na Serikali, Jeshi la Polisi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi yao ni kutaka kutwaa Umeya wa Jiji la Dar es Salaam lakini wataachia
“Watake wasitake wataachia, hapa ni Ukawa tu. Yote haya yana mwisho lakini wajue kuwa namba ‘zinatufeva’ na si vinginevyo,” amesema Mdee.
Mdee, Mwita Waitara ambaye ni Mbunge wa Ukonga na washitakiwa wengine watatu leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu na kisha kuachwa kwa dhamana.
Washitakiwa hao wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumjeruhi Terresia Mmbando ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliofanyika Jumamosi wiki iliyopita na baadaye kuhairishwa na kuibua malumbano ya kisiasa.
Washitakiwa wengine kwenye tuhuma hizo ni Shafii Juma, Alfonce Kinyafu, Manase John pamoja na Diwani wa Kimara Stop-Over ambapo kila mmoja amejidhamini mwenyewe kwa Sh. 2,000,000.
Mawakili wa wanasiasa hao ni Peter Kibatala, John Malya, Omari Msemo na Fredrick Kiwelo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mdee amesema, Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imedai kuwa, hakukuwa na sababu ya kuwakamata isipokuwa ni amri kutoka kwa viongozi wao.
Mdee amesema, jeshi hilo linaendeshwa kinyume cha sheria na kwa matakwa ya wanasiasa na watawala.
“Rais John Magufuli atake asitake ni lazima ataongozwa na Ukawa kwenye Jiji la Dar es Salaam na uchaguzi huu ni lazima Ukawa itashinda kwasababu namba haziwezi kubadilika,” amesema.
Amesema, mahakama imeweka wazi zuio la uchaguzi wa uchaguzi walilopeleka CCM sio halali na kwamba, (CCM) walikua wanatafuta njia ya kuiba kura katika uchaguzi huo.
Waitala ambaye ni Mbunge wa Ukonga amesema hatishwi na kuwekwa rumande na kwamba, wao kuwekwa huko ni sawa na simu iliyoisha chaji na kuchajiwa upya.
“Msimamo umeongezeka, wasimamizi wajipange kwani ukweli upo wazi sasa hakuna figisu,” amesema.
Wafuasi wa Chadema waliofika mahakamani hapo walishangilia kupewa dhamana kwa viongozi wao huku wakiimba ‘Peoples Power.’
Salum Mwalimu, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema amewapongeza watuhumiwa hao na kusema kuwa, hiyo ni moja ya changamoto za ukombozi.
“Tayari tumesikia kuwa wanabuni mbinu mpya ya kuwakamata madiwani ili kuitisha uchaguzi kwa kushtukiza,” amesema.
Mwalimu amesema, chama hicho kimepoteza wanachama wengi kwa kuuawa na wengine wamesingiziwa kesi hatimaye kufungwa.
Kesi hiyo iliyo chini ya Hakimu Mfawithi Mwanaamina Kumbakono, imepangwa kusikilizwa tena tarehe 16 Machi mwaka huu.
Chanzo:Mwanahalisionline1
Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee (wa pili kushoto), Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (wa tatu kutoka kushoto) na Diwani wa Kata ya Saranga, Ephrein Kinyafu (kulia) wakiwa ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Leo kabla ya kuanza kusikiliza kesi inayowakabili. 
3
Mbunge wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule, akiwa ndani ya mahakama ya mkazi kisutu kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo.
2
Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya akiwa na Katibu Mkuu, Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) wakisubiri kusikilizwa kwa kesi hiyo
4
5
6
7
8
9


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo