Mbunge wa Kawe Halima Mdee na wenzake wanne wamefikishwa mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam na kusomewa shitaka moja la kumjeruhi katibu tawala wa mkoa wa Dar es salaam
Halima Mdee akiwa na mbunge mwenzie Mwita Waitara wa jimbo la Ukonga pamoja na makada wengine watatu wa Chadema wamekana shitaka hilo na wametakiwa kujidhamini wenyewe kwa kiasi cha Shilingi Milioni mbili kila mmoja.
Mahakama hiyo imewaachia kwa dhamana baada ya kuweza kujidhamini