Timu ya Azam FC ilipoondoka jijini Johannesburg na kuwasili Dar es Salaam leo saa 12.15 jioni ikitoka kufanya makubwa nchini Afrika Kusini kwa kuichapa Bidvest Wits mabao 3-0 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Baadhi ya picha zinawaonyesha baadhi ya mashabiki wa Azam FC walioipokea timu yao kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere (JNIA)
Azam FC itarudiana na Bidvest Wits +Jumapili ijayo (Machi 20) mchezo utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex kuanzia saa 9.00 Alasiri.