Tume ya Ushindani kwa kushirikiana na jeshi la Polisi leo wameendesha Operesheni ya kukamata simu Bandia aina ya Samsung katika mitaa mbalimbali ya Karikaoo jijini dsm baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wakala wa Samsung Protection Agency.
Katika Msako huo uliohusisha maduka kadhaa zaidi ya simu 592 zenye thamani ya shilingi millioni 44.4 zimekamatwa pamoja na baadhi ya wauzaji wa maduka hayo na kufikishwa katika kituo cha polisi cha Msimbazi kwa ajili ya hatua zaidi ikiwemo kuchunguza na kubaini ziliingizwa vipi katika soko.
Afisa Uhusiano wa Tume ya Ushindani Frank Mdimi amesema kampuni ya Anti- Illicit Agency ambayo ni wakala Samsung amesema baada ya kufanya Uchunguzi walibani baadhi ya wenye maduka wamekuwa wakiuza simu hizo kinyume cha sheria za tume ya Ushindani.