Mkuu wa wilaya Ashtakiwa

Wakazi wa Kijiji cha Monze, Manispaa ya Ilemela, Mwanza wamemshutumu Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Manju Msambia kutoa kibali cha kufungwa kwa barabara ya Uwanja wa Ndege, Igombe bila kuwashirikisha.

Msambia alikiri kuandika barua kufunga barabara hiyo, akisema ni maagizo ya Serikali. Wananchi hao walisema hayo juzi mbele ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela. 

Mkazi wa kijiji hicho, Tito Kihomole alisema wameachwa kisiwani kama siyo wananchi wa Tanzania, kwani barabara hiyo ina umuhimu kwao na kwamba kufungwa ni kuwakandamiza. 

Mkazi mwingine, Grace Leopodi alisema hata wanafunzi wanachelewa kufika shule kwa wakati kutokana na adha hiyo. 

Diwani wa Kata ya Shibula, Dede Swira alisema kufungwa kwa barabara hiyo kutarudisha matatizo kwa wananchi hasa wajawazito ambao wanatembea umbali mrefu kufika kwenye kituo cha afya.  


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo