Madiwani Makete waazimia kula sahani moja na Mkuu wa Mkoa wa Njombe

Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe wameunga mkono kauli aliyoitoa mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi aliyoitoa katika baraza lao kuhusu kaya zote masikini wilayani Makete kuunganishwa na mfuko wa afya ya jamii CHF

Kuunganishwa kwa kaya hizo katika mfuko wa CHF kutawezesha kaya hizo kupatiwa matibabu bure kwa muda wa mwaka mzima kwa gharama ya shilingi 10,000/= ambapo atatibiwa mkuu wa kaya na wategemezi wake

Akizungumza na mtandao huu diwani wa kata ya Ipelele kupitia CHADEMA Mh. Mwipelele Mbogela amesema bila kujali itikadi ya vyama anaunga mkono wazo la mkuu wa mkoa kwa kuwa litasaidia kunusuru hali ya umasikinini iliyowaelemea wananchi na hivyo itasaidia kupunguza kiwango kikubwa cha fedha wanachotumia kwa ajili ya matibabu

Amesema kwa maisha ya sasa kaya masikini zinasaidiwa na mfuko wa maendeleo ya jamii wa TASAF awamu ya tatu na wakati wa ukauagi kaya hizo wapo wengi waliobainika kutumia fedha hizo kwa ajili ya matibabu, hivyo njia nzuri ya kupunguza wao kutumia fedha hizo kwa ajili ya matibabu ni kuwaunganisha na mfuko wa afya ya jamii CHF

Kwa upande wake diwani wa kata ya Ukwama kupitia CCM Mh Augustino Tweve amesema baada ya baraza hilo kumalizika akifika kwenye kata yake ni hamasa huku akiwashirikisha wadau wa maendeleo katika kata yake wakiwemo wa nje kuchagia kwa kadri ya uwezo wake ili kaya zote masikini katika kata yake ziunganishwe na CHF

"Wazo la mkuu wa mkoa ni zuri kabisa, kaya masikini zinasumbuliwa sana na maradhi hivyo kama tutapata michango ya kutosha kutoka kwa wananchi wenye uwezo na wadau wa maendeleo kutapata fedha za kutosha kuwaunganisha wote na CHF, mimi nitaonesha mfano katika kata yangu" amesema diwani huyo

Aidha katika baraza hilo mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi aliahidi kutoa zawadi ya pikipiki moja kwa halmashauri itakayokuwa ya kwanza kuziunganisha kata zote masikini na mfuko wa bima ya afya wa CHF katika mkoa wake


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo