Shirika la TAFEYOCO (Tanzania Feminist and Youth Change Organization)
linalojihusisha na maswala ya Wanawake na vijana katika kutatua
changamoto zao kiuchumi, kisiasa na kijamii limemuomba Mhe Rais apange
muda wa kuonana na vijana wa mkoa wa Dar es salaam kama alivyofanya kwa
wazee.
Wakizungumza
jijini Dar es Salaam mapema leo Februari 18, vijana hao kupitia
Mwenyekiti wao Elvice John Makumbo wamebainisha kuwa miaka yote viongozi
wa nchi ukutana na wazee na kusikiliza changamoto zao lakini kwa sasa
Tanzania idadi kubwa ya watu ni vijana na ndio waliokuwa wanakesha na
kuyalilia mabadiriko haya tunayoyaona kipindi hiki hivyo tunamuomba Mhe
Rais akutane na vijana na kusikiliza changamoto zao na ushauri kwenye
utendaji wake.
Tazama hapa kupitia Mo tv Online