Na”George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mwenyekiti wa
Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoa wa Mwanza Makoye Kayanda Bunoro
anawatakia Waendesha Pikipiki wote nchini Kheri ya Mwaka Mpya 2016 huku
akiwasihi kutimiza majukumu yao kwa kufuata sheria na taratibu za
Usalama barabarani bila shuruti.
“Tuache
Mchezo na Vyombo vya Moto, Tuvae Elmenti, tusibebe mishkaki (zaidi ya
abiria mmoja) tusiendeshe kwa mwendo kasi kwani ni hatari, tusitumie
pombe tukiwa kazini huku tikiwapenda abiria na kujiepusha na vitendo vya
uhalifu vya aina yoyote”. Anasema Bunoro.
Aidha
Bunoro amewaomba radhi wale wote waliopata usumbufu kwa namna moja ama
nyingine kutokana na kazi ya bodaboda na kwamba kusameheana ndilo jambo
la msingi huku akiwakumbusha bodaboda kujipanga katika majukumu yao ili
kuendana na kasi ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli ya “Hapa Kazi Tu”.
Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi