Mtuhumiwa awatumia polisi selfie yake ili wamtafute vizuri

Ikitokea unakutana na ripoti kwenye kona yoyote kwamba unatafutwa na Polisi lazima mapigo ya moyo yaanze kwenda kasi… kama ni kesi, unatafutwa kwa kesi gani? Hilo swali halitokosa kujiuliza, lakini jamaa wa Marekani kaona isiwe tabu, hajapenda picha yake ambayo Polisi wameitumia kutangaza sura yake kwamba anatafutwa, akatwanga selfie yake alafu akawatumia Polisi.
Kwa ujasiri wake wote na kuonesha kwamba hakuwa anatania akaamua kuwaandikia kabisa >>> ‘Picha hii iko poa zaidi kuliko hiyo mliyotumia
Jamaa huyo Donald “Chip” Pugh kwa bahati nzuri alipatikana kwa njia ya simu akafanyiwa interview kwenye radio moja, akalalamika kwamba picha waliyotumia Polisi ni ya ovyo kabisa wala hakuipenda… walipomuuliza yuko maeneo gani jamaa akagoma kabisa kujibu.
Donald kutoka  Lima, Ohio Marekani alikuwa na kesi na alitakiwa kuripoti Polisi, lakini kwa sababu hakutokea Kituo cha Polisi, jamaa wakaweka picha yake kwenye ukurasa wa Facebook ambayo yeye hakuipenda, akapiga selfie akawatumia ili waitumie hiyo kutangaza wanamtafuta.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo