CCM waomba msamaha kwa watanzania

TAARIFA KWA UMMA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa sana na ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi ulioandikwa kwenye moja ya Bango lililobebwa na mmoja wa wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaomba radhi kwa ujumbe huo, kinapinga na kinakemea kabisa fikra, hisia na mitazamo yoyote yenye maudhui ya kibaguzi.


Ujumbe huo sio tu kuwa una maudhui ya kibaguzi bali pia unaenda kinyume kabisa na falsafa na Shabaha ya waasisi wa Mapinduzi hayo Matukufu ya mwaka 1964 na unapingana na misingi na itikadi ya CCM inayohimiza Umoja na Mshikamano wa Kitaifa.

Daniel Chongolo
Mkuu wa Mawasiliano na Umma CCM.
12/01/2016

TAARIFA KWA UMMAChama Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa sana na ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi ulioandikwa kwenye...
Posted by Chama Cha Mapinduzi on Tuesday, January 12, 2016


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo