Abiria waliokuwa wakisafiri kutoka na kwenda Njombe na mkoa jirani wa Mbeya pamoja na watumiaji wengine wa barabara, jana wamekiona cha moto baada ya kusota eneo la Luchala kijiji cha Ikonda kata ya Tandala kwa zaidi ya saa 8 kutokana na lori lililokuwa limebeba mali za serikali kukwama na kuziba barabara
Tukio hilo la aina yake limesababishwa na ukubwa wa lori hilo hasa ukizingatia kwamba udogo wa Makete ni wa mfinyanzi na hivyo kuwa na utelezi hasa ukinyeshewa na mvua kama ilivyotokea jana
hata hivyo lori hilo lilivutwa eneo hilo majira ya saa nne usiku na kusababisha mawasiliano ya barabara hiyo kurejea kama kawaida, huku abiria wakitumia bodaboda kwenda kwenye maeneo wanayotaka kufika pamoja na mabasi yaliyokuwa ng'ambo ya pili kulazimika kurudi na abiria yalikotoka, hasa yaliyokuwa yakienda Makete mjini
Hizi hapa chini ni picha za tukio hilo
abiria wakitembea kwa miguu kutafuta usafiri wa kuwafikisha Makete mjini na Bulongwa
Basi la Mwafrika likiwa limesimama baada ya kushindwa kupita eneo hilo
Lori lililofunga barabara baada ya kukwamakazi kweli kweli
Abiria wakiangalia nafasi kwenye basi hili
Wazee wangu hawa daaah hadi huruma, ni mwendo wa kutembea kwa miguu
Barabara ndio imefungwa kwa namna hii
Bodaboda nayo ikiteleza kwenye eneo hilo
Wanafunzi wakitembea kwa miguu angalau wawahi wakaripoti shuleni
Gari dogo likijitahidi kupenya pembeni mwa lori lililofunga barabara