Zoezi
la bomoabomoa kwa wakazi wa mabonde ya Kinondoni limesitishwa mpaka
kesi ya msingi itakaposikilizwa katika mahakama kuu ya ardhi.
Jaji
wa mahakama kuu ya ardhi amemtaka wakili wa walalamikaji kuwasilisha
mapema orodha ya walalamikaji wote 674 na majina yao kamili,anuani za
makazi na nyumba zao na kisha shauli hilo litafikishwa Jumatatu, 11
January kwa ajili ya kupangiwa tarehe ya shauli lao.
Baada
ya kutolewa kwa hukumu hiyo ya kusimamisha zoezi la uvunjaji wa nyumba
katika mabonde hayo wakazi wa mabondeni wameonekana kuwa wenye furaha na
kushangilia kusimamishwa kwa zoezi hilo.
