Waziri Nape Akanusha Wizara Yake Kukataza Wanawake Kuvaa Mavazi ya Kubana na Vimini

Waziri wa Habari, Utamaduni Wasanii na Michezo Nape Nnauye, amekanusha taarifa iliyosambaa mitandaoni inayohusu wizara yake kukataza baadhi ya mavazi hasa sehemu za mikusanyiko ya umma.

Amesema Taarifa hizo ni za uzushi na uongo, na kuwataka mamlaka husika kuwachukulia hatua watu waliotoa taarifa za uongo.

“Hizo taarifa ni uzushi mtupu na uongo, mamlaka husika wachukue hatua, watimize wajibu wao, watumie sheria iliyopo kuwachukulia hatua”, amesema Mh. Nape Nnauye.

Mwishoni mwa wiki hii kuna taarifa ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha ni taarifa kwa vyombo habari juu ya katazo la mavazi yasiyofaa kwenye mikusanyiko ya watu, hususan hospitali, maofisini, sokoni, na vyuoni.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo