Kukithiri kwa biashara haramu ya ngono pamoja na tabia ya ushoga
mkoani Iringa kunadaiwa kusababishwa na baadhi ya vijana wa vyuo vikuu
wanafika mkoani humo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu, huku miongoni
mwao wakitaka starehe zilizo nje ya uwezo wao.
Tamaa ya kumiliki vitu vya thamani – ni miongoni mwa mambo
yanayotajwa kuwahadaa baadhi ya wasomi hao wa vyuo vikuu, jambo
linalosababisha wengi wao kuangukia katika wimbi la biashara ya ngono na
ushoga na kuufanya ongezeko la maambukzi ya vvu.
Kwa mkoa wa iringa inadaiwa kuwa zaidi ya mashoga 1500 wamejitangaza
wenyewe kuendesha biashara haramu ya ngono, jambo ambalo kiafya
linadaiwa kuwa ni hatari kwa maambukizi ya virus vya ukimwi.
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani iringa
ndiyo wanaonyooshewa kidole kuhusika na biashara hiyo ya ngono na tabia
ya ushoga- ambapo shirika la restless development linalojihusisha na
masuala ya afya ya uzazi na makuzi kwa vijana- kupitia mradi wa dance
for life- limewakutanisha viongozi hawa wa serikali ya wanafunzi wa vyuo
vikuu mkoani iringa- ili kujadili namna ya kujinasua katika wimbi hilo
la ushoga na biashara haramu ya ngono.
Serikali inaona tatizo hilo la ushoga na biashara ya ngono
litamalizwa na jamii yenyewe, endapo tu wazazi na walezi watakemea
mapema mienendo hatarishi ya vijana wao.
Ushoga ni tabia inayofanywa na baadhi ya wanaume, kwa kujihusisha
kimapenzi na wanaume wenzao, suala ambalo kwa kiwango kikubwa linatajwa
kuchochewa na mambo ya utandawazi, ambao unaibua mitindo mbalimbali na
tabia mpya kila uchwao.