SPIKA wa Bunge, Job Ndugai ameeleza kusikitishwa na taarifa
zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na katika baadhi ya vyombo vya
habari zikieleza kuwa ni mgonjwa mahututi.
Akizungumza juzi kwa simu kutokea India, mmoja wa wasaidizi wa Ndugai, Lukindo Choholo, alisema taarifa hizo zimemsikitisha kwa sababu anaamini wanaozisambaza wana lengo la kupotosha jamii.
Choholo alisema Ndugai ambaye yuko nchini
India kwa uchunguzi wa macho, amekuwa akifuatilia taarifa zinazomhusisha
na kuugua maradhi ya figo na ini, huku wanaozisambaza wakiwa hawana
taarifa za uhakika kuhusu mwenendo wa afya yake.
“Habari zinazosambazwa huko nyumbani kwenye mitandao ya kijamii na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa Spika Ndugai ni mgonjwa sana zinamsikitisha sana, anafuatilia kwenye mitandao na magazeti pia.