Katika hatua nyingine katibu mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema, Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma.
Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.
Balozi Sefue amewataka watumishi wengine wa umma kutii agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kuonya kuwa atakayekiuka atachukuliwa hatua kali.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
16 Desemba, 2015
BONYEZA PICHA HAPO CHINI KUSIKILIZA SAUTI YA IKULU KUHUSU UAMUZI HUO WA MH. RAIS
BONYEZA PICHA HAPO CHINI KUSIKILIZA SAUTI YA IKULU KUHUSU UAMUZI HUO WA MH. RAIS
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, akiongelea utenguzi wa Mkurugenzi wa TAKUKURU Dk. Edward Hosea uliofanywa na Rais Magufuli na pia kusimamishwa kazi kwa watumishi wanne wa TAKUKURU ambao waliomba kibali cha kusafiri nje ya nchi na kukataliwa lakini wakaamua kusafiri kibabe. (AUDIO) Usisahau kuSHARE na marafiki
Posted by East Africa Television (EATV) on Wednesday, December 16, 2015
