Msichana wa miaka 18 mbaroni kwa kuwafanyisha ukahaba watoto huko Singida

Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 18 anashikiliwa na Polisi mkoani Singida kwa tuhuma za kuwashawishi watoto wa kike na kuwafanyisha biashara ya ngono kwa ujira wa kati ya shilingi 3,000 na 5,000 suala ambalo ni kinyume cha sheria, ukatili na ukiukaji wa misingi ya haki za binadamu.
Mtuhumiwa huyo Mastura Saidi mkazi wa Karakana Mjini Singida amekamatwa Jumatatu hii majira ya saa mbili usiku baada ya watoto watatu mwenye umri kati ya miaka 12 na 15 kukutwa ndani ya chumba chake wakiwa na madereva wa bodaboda wakiendelea kufanya nao mapenzi.
 Katika kituo kikuu cha Polisi Mjini Singida Kamanda wa Jeshi hilo ACP Thobias Sedoyeka amekutana na waandishi wa habari kutoa taarifa za watoto watatu wanafunzi wa shule msingi kukutwa kwenye chumba kimoja wakiwa na madereva bodaboda wakifanyishwa biashara ya ngono.
Amesema wakati watoto hao wakifanyiwa uchunguzi wa afya zao, msichana anayetuhumiwa kuwafanyisha biashara hiyo pamoja na madereva watatu wa bobadoda waliofanya nao mapenzi wanashikiliwa na Polisi.
Kamanda Sedoyeka amesema watuhumiwa hao watakabiliwa na mashitaka mbalimbali.
Baadhi watoto waliotendewa unyama huo pamoja na madereva bobaboda wanaotuhumiwa kufanya nao mapenzi wanaeleza kilichotokea hadi kujikuta wakiwa mikononi mwa jeshi la Polisi.
Hata hivyo mtuhumiwa wa kwanza anayedaiwa kuwakusanya watoto hao kwenye chumba chake na kuwatafutia wanaume kwa ujiri wa kati ya shilingi 3,000 na 5, 000 anakanusha vikali madai hayo.
Hili ni tukio la pili la aina hii kutokea Mjini Singida ambapo mwaka juzi watoto wengine 13 wa kike na kiume wenye umri wa kati ya miaka 12 na 15 walikamakatwa usiku wa manane kwenye chumba kimoja eneo la bima wakidaiwa kujihusisha na vitendo vya mapenzi katika umri mdogo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo