Msanii wa Bongo Fleva kunusurika kuuawa baada ya kuitwa mwizi

Rapper kutoka kwenye zao la Serengeti Fiesta Supa Nyota 2013, Edu Boy amenusurika kifo baada ya kuitwa mwizi maeneo ya Sinza wakati akitoka studio za Freenation kurekodi ngoma.
Msanii huyo akiongea kwenye Clouds TV alisema…’Nilikuwa natoka studio kurekodi ngoma ilikuwa usiku nikakutana na vijana watano wakanisimamisha wakaniuliza kuna mtu umekutana naye nikajibu sijakutana na mtu mmoja wao akasema ndio huyu huyu,ghafla nikashangaa napigwa ngumi na mateke’>>> Edu Boy
‘Wakaniambia kuna mama kaibiwa kwahiyo mimi ndio mwizi wakanipiga sana na kunipora pesa na simu,bahati nzuri kuna jamaa alikuwa ananijua wakati watu wanabishana ili waniue akaniambia nipitie kichochoroni nikimbie, nikafanikiwa kujiokoa lakini nilikuwa na hali mbaya’>>>Edu Boy
Edu Boy amesema kuwa alitoa taarifa Polisi na kupewa PF3 na kutibiwa na kesho yake askari waliweza kufika eneo la tukio na kufanikiwa kuwatambua wahusika na wamefikishwa kwenye vyombo vya dola na kufunguliwa mashtaka.
Chanzo:Millardayo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo