Mkazi wa Kijiji cha Irogero, Kata ya Kamachumu
wilayani Muleba, Archard Fredrick, anadaiwa kuuawa na mkewe kwa kupigwa na nondo kichwani akiwa amelala.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi alisema
jana kuwa mtuhumiwa amelazwa Hospitali ya Ndorage akiwa
chini ya ulinzi wa polisi kwa kosa la kujaribu kujiua kwa kunywa
sumu baada ya tukio.
Ollomi alisema, mtuhumiwa aliuchukua mwili huo na kwenda
kuufunika kwa majani ya migomba kwenye shamba lao jirani na nyumba yao.
“Uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia,” alidai
kamanda huyo.
Katika tukio lingine, Kamanda Ollomi alisema polisi wanamsaka mkazi mmoja wa Kijiji cha
Nyaruzumbura, Tarafa ya Kaisho wilayani Kyerwa kwa tuhuma za kumuua mtoto wake kwa
kumshmabulia kwa kumkata na panga kichwani.
Chanzo cha mauaji hayo inadaiwa kuwa ni ulevi wa pombe.
Mtoto huyo alifariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Nkwenda.