Mnyika akerwa na Waziri...amuomba Waziri Mkuu aingilie kati

MBUNGE wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika amemuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufanya ziara katika ofisi za Dawasa na Dawasco ili ‘kutumbua majipu’ ya yaliyopo katika taasisi hizo za umma. 

Mnyika ambaye ni Mbunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alidai jana kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo ya kumuomba Waziri Mkuu kuingilia kati tatizo hilo, baada ya kutoridhishwa na hatua alizochukua Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa baada ya kufanya ziara alipoteuliwa.


“Sijaridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Waziri wa Maji alipofanya ziara juzi na kunukuliwa na vyombo vya habari. Hivyo, naomba Waziri Mkuu achukue hatua zifuatazo,” ilisema sehemu ya taarifa ya Mnyika kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana.



Mbunge huyo wa Chadema aliomba Waziri Mkuu, aitake Wizara ya Maji na Umwagiliaji impatie nakala ya ripoti ya uchunguzi kuhusu kukatikakatika mara kwa mara kwa maji katika mitambo na maeneo ambayo yanahudumiwa na mitambo ya Ruvu Juu.



Baada ya kupatiwa ripoti hiyo, Mnyika alisema Waziri Mkuu afanye ziara katika ofisi za Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) na Shirika la Majisafi na Majitaka (DAWASCO) na ‘kutumbua majipu’ ya ufisadi na udhaifu yaliyopo katika ofisi hizo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo