Madiwani wawili wa chama cha demakrasia na
maendeleo (Chadema), wanahojiwa na Polisi mkoani
Kilimanjaro kwa tuhuma zinazoangukia katika makosa
ya jinai.
Mmoja wa Madiwani hao kutoka Halmashauri ya Wilaya
ya Rombo, anahojiwa kwa tuhuma za kutishia kumuua
kwa maneno, mbunge wa Jimbo hilo Joseph Selasini.
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro,Flugence
Ngonyani,jana alilithibitishia gazeti hili kukamatwa kwa madiwani hao kwa nyakati tofauti
na kuhojiwa kisha kuachiwa kwa dhamana
Ngonyani alisema Diwani wa kata moja ya wilaya ya Rombo(Jina linahifadhiwa)
alifunguliwa shauri na mbunge Selasini, kwa kile alichodai kuwa alimtishia kumuua kwa
maneno.
Kamanda Ngonyani alisema Mbunge huyo aliandika maelezo ya kuwa Diwani huyo
alitishia kumuua na kwamba upelelezi juu ya tuhuma hizo umeanza.
Pia Diwani mwingine katika Manispaa ya Moshi,nae alishtakiwa kwa kosa la kumsambulia
mkazi wa kata take na kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwili.
Kamanda alisema kuwa uchunguzi unaendelea ili kuweza kubaini kiini halisi cha ugomvi
na kwamba watafikishwa mahakama upelelezi utakapo kamilika.
Hata hivyo kamanda Ngonyani hakufafanua ni lini matukio hayo yalitokea zaidi ya kusema
Diwani wa Rombo alikamatwa mwishoni mwa wiki na yule wa Moshi mjini alikamatwa
jana.
