Kuanzia sasa muziki utakaopigwa kwenye vyombo vya habari lazima upitie COSOTA upewe kibali

Serikali imetoa tamko kwa vyombo vyote vya habari nchini kuanzia january mosi mwakani kutotumia miziki ya aina yeyote ,wa ndani au nje bila kibali kutoka Cosota.

Wakitoa tamko hilo kwa pamoja waziri wa habari michezo na utamaduni Nape Nnauye na waziri wa viwanda na biashara Charles Mwijage wamewataka wamiliki wa vyombo vya habari kutoa ushirikiano.

Nape amesema atalisimamia zoezi hilo na kutoa tahadhari kwa chombo chochote cha habari kitachokiuka tamko hilo hatakionea haya kukifungia leseni.

Naye waziri wa viwanda na biashara amesema kuna kampuni ya wazawa ya CMEA ambayo imeanza kazi ya kusimika mitambo yake  kila mkoa itakayofanya kazi ya kunakili kila kinachofanyika kwenye kila chombo cha habari.

Kwa upande wa wasanii msanii Nick wa pili amependekeza muziki wa wasanii wa nje ya tanzania uchajiwe gharama kubwa ili muziki wa Tanzania upate nafasi kubwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo