Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la
Flora Msigwa anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Njombe kwa tuhuma za kuiba mtoto
wa Irene Kayombo mkazi wa Njombe
Kamanda wa polisi mkoani Njombe
Wilbroad Mutafungwa amekiri kumshikilia mwanamke huyo na kwamba mara
baada ya kupewa taarifa za mama huyo kuwa na mtoto mchanga wasamaria wema
walitoa taarifa kituo cha polisi Makambako ambako jeshi hilo lilifika kwake na
kumkuta mtoto huyo akiwa naye na alikiri kutenda kosa hilo.
Mtuhumiwa aliiba mtoto huyo
katika hospitali ya Kibena Njombe ambapo mama wa mtoto alikuwa akimuuguza dada
yake.