Wanachama wa CUF watifuana huko Tanga

Wanachama  zaidi ya mia moja wa chama cha wananchi CUF wilaya ya Pangani Mkoani Tanga wametishia kujeresha kadi zao za chama na kujiunga na vyama vingine vya siasa..
Madai ya wanachama hao ni kutaka kurejeshwa kwa jina la aliyekuwa mbunge wa viti maalumu Amina Mwidau kwa kuwa ndiye aliyeshinda kwenye kura za maoni na kuliondoa jina na Saumu Sakala aliyeshika nafasi ya pili kwenye mchakato wa kura za maoni.
 Wananchi wa chama cha wanchi CUF waliokuwa wakitishia kukihama chama hicho kufuatia kutorejeshwa kwa jina la Aliyekuwa mbunge wa viti Maalumu Amina Mwidau.
Wanachama hao wanasema chama hicho kinaweza kufa kama uongozi wa juu hautasikia kilio hicho chenye maslahi ya kisiasa katika wilaya ya Pangani.
 Katubu wa chama hicho wilaya ya Pangani Ramadhan Hadadi amesema waliofanya kazi hiyo ni Baraza la uongozi la chama hicho Taifa.
Amina Widau licha ya kugombea viti maalumu kupitia chama hicho  ,aligombea kwenye jimbo la Pangani na kuangushwa na mgombea CCM Jumaa Aweso.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo