Walionusurika kifo mgodini kwa kukaa siku 41 sasa kupakwa kinyesi


Wazee wa kimila wa makabila ya Wakurya na Waluo wamesema watu watano waliookolewa kutoka kwenye machimbo ya Nyangalata, Kahama ambao waliwekewa matanga kabla ya kuibuka wanatakiwa kufanyiwa mambo ya kimila, vinginevyo watakufa kiajabu.

Mmoja wa wazee hao, Ghati Ryoba (61) wa Mtaa wa Mwangaza, Nyamisangura – Tarime amesema: “Mtu akidaiwa kuwa amekufa lakini baadaye akaonekana, wazee wa ukoo au wa mila humfanyia matambiko kama njia ya kuondoa mikosi kwake na kwa familia yake. Wanachukua kondoo mweusi wanamchinja kisha wanamtambikia (bharamsendola).

“Kisha wanachukua kinyesi cha kondoo (ubhuhu ghwaling’ondi) na mti mmoja unaitwa (richirya) kisha kile kinyesi kinarushwarushwa ndani ya nyumba yake na mji mzima kama kuna nyumba nyingine halafu wanachukua kile kinyesi cha kondoo na kumpaka kwenye mikono na anashikana mikono na watu.”

Mzee huyo wa kimila ameongeza kusema kuwa baada ya hapo atanawa mikono kabla ya kuruhusiwa kula na kujumuika na watu.

Amesema baada ya hapo atanyolewa kisha atakwenda kuoga “... Wengine hupeleka nywele kuzizindika kwenye mlima ambako watu hawalimi.”

Kuhusu Waluo, mzee Peter Odello wa Kitembe, Rorya amesema:“Kama inatokea mtu anadaiwa kufa na watu wakafanya matanga lakini baadaye akaonekana, lazima arudi kijijini wamfanyie matambiko.”

Amesema akirudi, wazee watachinja ng’ombe na watu watakaa tena kama walivyokaa kwenye matanga kwa siku mbili au tatu watu wakila kisha kupewa dawa inayoitwa manyasi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo