Wanachama wa Chama cha Mapinduzi waliokisaliti Chama hicho katika uchaguzi Mkuu wilayani Urambo mkoani Tabora wametakiwa kujiondoaa wenyewe kabla ya kuondolewa kwa nguvu.
Agizo hilo limetolewa na uongozi wa CCM katika hafla ya kuwashukuru wananchi kwa kukipa ushindi chama hicho kwenye uchaguzi uliomfanya Dokta John Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Magreth Sitta kuwa Mbunge wa Urambo.
Chama cha Mapinduzi Wilayani Urambo kinafanya uungwana wa kuwashukuru wananchi ambao wanaombwa radhi pale walipokwazwa wakati wa kampeni.
Ahadi nyingi zilitolewa wakati wa kampeni ambazo wananchi wanaondolewa hofu na kwamba zitatekelezwa.
Mbunge mteule Magreth Sitta anakuwa wa kwanza Mkoani Tabora kuwashukuru wananchi wa kata zote kwenye jimbo muda mfupi baada ya uchaguzi mkuu.