Tanesco yafanya operesheni kagua mita usiku


Shirika la Umeme (Tanesco) limesema kutokana na kukithiri kwa wizi umeme kunakofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu, shirika hilo limelazimika kufanya operesheni ya kukagua mita za umeme kwenye nyumba za wateja wao usiku.

Akizungumza kufuatia tangazo la Shirika hilo la kuanza ukaguzi wa mita zake lililotolewa wiki mbili zilizopita, Msemaji wa Tanesco, Adrian Severine, alisema uamuzi wa kukagua mita usiku umetokana na changamoto wanayokabiliana nayo operesheni hiyo inapofanyika mchana.

Alisema wafanyakazi wao wanapofika kwenye nyumba za wateja wao wanakosa ushirikiano kwa kuwa wenye nyumba wanakuwa kazini na nyumbani wanabaki wasaidizi ambao hukatazwa na waajiri wao kuwafungulia nyumba.

"Imetulazimu kuwavizia wateja majira ya usiku muda ambao wanakuwa wamesharudi kutoka kazini ili tuweze kukagua mita," alisema.

Aliongeza kuwa baada ya ukaguzi huo wakibaini kuna wizi umefanyika huwakamata kwa kushirikana na polisi na kufikishwa kituoni kwa ajili ya hatua nyingine.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo