Taarifa nyingine kutoka Ikulu muda huu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anamtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Chama Cha Madereva Tanzania (TADWU) kufuatia kifo cha aliyekua Katibu Mkuu wa Chama hicho Bw. Rashid Salehe kilichotokea Tarehe 20 Novemba, 2015 katika Hospitali ya Taifa Mhimbili.
Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema taifa limempoteza mtu shupavu, mkweli, makini na aliyependa kupigania haki pale alipoamini kuwa panastahili haki hiyo na alithibitisha kwa kupigania uanzishwaji wa Chama Cha Madereva na kusimama kidete kutetea haki zao.
"Nawatakia moyo wa uvumilivu familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki,  madereva na wengine wote ambao wameguswa na kifo cha Rashid Salehe na wote tuungane kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ampumzishe mahali pema peponi"
Dr Magufuli anaungana na wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki kigumu na kwamba taifa litauenzi mchango mkubwa alioutoa marehemu Rashid Salehe.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi Mawasiliano, IKULU
23 Novemba, 2015 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo