Serikali yapiga marufuku kutumia ramani ya Tanzania isiyo sahihi

Ramani rasmi ya Tanzania iliyotolewa na Serikali mwaka 2013


SERIKALI imesema itavichukulia hatua vyombo vya habari pamoja na watu watakaobainika kutumia ramani ya Tanzania ambayo sio sahihi.



Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene, alisema kumekuwa na matumizi ya ramani ya Tanzania ambayo inaonesha Ziwa Nyasa lipo katika nchi ya Malawi pekee huku Tanzania ikionekana kutohusika kabisa katika ziwa hilo.



Mwambene alisema ramani sahihi ya Tanzania inaonesha Ziwa Nyasa lina mpaka katikati ambao unaonesha umiliki wa ziwa hilo upo upande waTanzania na Malawi. Aliongeza kuwa hivi karibuni kumekuwa na vyombo vya habari ambayo vimekuwa vikitumia ramani hiyo ambayo sio ramani sahihi.



“Ni vibaya sana vyombo vya habari kutumia ramani ambayo sio sahihi kwani kufanya hivi ni kuharibu utaifa na utambulisho wetu,” alisema Mwambene.



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo