Rais wa Tanzania mwaka 2050 huyu hapa

Mtoto Yusuph Nassoro (1 na miezi nane) akipunga mkono akiwa kwenye jukwaa alilojengewa ana baba yake mzee Nassoro Salum (69) mkazi wa Majengo mjini hapa. Mzee Nassoro amedai anamjengea mazingira mtoto wake huyo kitinda mimba, kuja kuwa Rais ifikapo mwaka 2050.
Alisema tayari wamemfungulia mtoto wao Yusuph akaunti kwenye benki ya CRDB tawi la Singida,lengo ni kuweka akiba ya fedha za kutosha kugharamia masomo yake.
“Kubwa zaidi ni kwamba mimi na mke wangu,tumeunganisha nguvu zetu kuhakikisha tunamlea Yusuph ipasavyo, ili aweze kukua katika maadili mema,awe mchapa kazi na asiye na makundi yasiyofaa”alisema.
Akifafanua zaidi,mzee Nassoro alisema pamoja na Yusuph kuwa na umri mdogo,ameshiriki kikamilifu mikutano yote ya kampeni ya CCM,lengo likiwa ni kumjengea mazingira mazuri aje kuwa mwana siasa mahiri na shupavu siku za usoni.
“Hivi sasa Yusuph akiona navaa nguo zangu za kijana,na yeye anaanza kutafuta za kwake za kijani.Akizinduka kutoka usingizini,akisikia wimbo wa CCM,anaanza kuruka ruka na kupunga mikono yake hweani (juu)”,alisema Mzee Nassoro.
Katika hatua nyingine,mzee huyo mfanyabiashara hapa mjini,amewataka wazazi/walezi kubadilika na kujenga utamaduni wa kulea ipasavyo na kuwasaidia watoto wao kutimiza ndoto/malengo yao ya muda mfupi na muda mrefu.
Kuhusu serikali mpya ya awamu ya tano,amemwomba Rais Magufuli,kuanzisha vyuo maalum kwa ajili ya kuwandaa vijana wadogo kuja kuwa viongozi bora,waadilifu,wachapa kazi na wabunifu wazuri kwa faida ya taifa hili.

DSCN5292
Mzee Nassoro Salum (69)  mkazi wa Majengo mjini hapa, akiwa na mtoto wake Yusuph (1 na miezi nane) akiwa ofisi ya klabu ya waandishi wa habari mjini Singida. Mzee Nassoro,amedai anamwandaa Yusuph kuja kuwa Rais mwaka 2050.
Katika kuhitimisha,mzee Nassoro alisema “Kama mnavyoniona,maisha yangu sasa yapo ukingoni na mtoto wangu kitinda mimba Yusuph bado mdogo mno.Naomba taasisi,asasi mbali mbali na mtu atakayejisikia kunisaidia kugharamia masomo ya mtoto huyu,anipigie no.0684  088  486”.
Alisema matarajio yao ni kumwanzisha Yusuph katika shule za awali zinazomilikiwa na madhehebu ya ndini kwa madai kuwa zinasimamia maadili kikamilifu.
Naye Naomi Ntembo mkazi wa Mitunduruni mjini hapa, pamoja na kumpongeza mzee Nassoro,ametumia fursa hiyo kuitaka jamii nchini kuiga mfano wa mzee huyo kuwalea vizuri watoto na kuwaandalia mazingira mazuri ya kutimiza ndoto au malengo yao.
DSCN5317
Mkazi wa Mitunduruni mjini Singida, Naomi Ntembo, amempongeza mzee Nassoro Salum kwa malengo yake ya kumlea na kumsomesha mtoto wake Yusuph ili aje kuwa Rais mwaka 2050. Ameitaka jamii kuiga mfano wa mzee Nassoro.
DSCN5323
Baadhi ya wakazi wa kata ya Ipembe mjini Singida, wakiwa wameungana na Watanzania, kufuatilia uapishwaji wa Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano jana.(Picha naNathaniel Limu).


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo