Mwendesha pikipiki auawa kinyama na kuporwa pikipiki yake huko Mbeya

MWENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA MKAZI WA MWAKA KATIKA MJI MDOGO WA TUNDUMA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JOHN SIMWITO KABUJE [22] AUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI UPANDE WA KUSHOTO NA KISHA  KUNYANG’ANYWA PIKIPIKI AMBAYO BADO KUFAHAMIKA NAMBA ZA USAJILI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 23.11.2015 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO MTAA WA MAPOROMOKO, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. 

INADAIWA KUWA, MAREHEMU AKIWA NA KATIKA KAZI YAKE, ALIKODIWA NA MTU MMOJA NA WAKATI WAKIWA NJIANI WALIJITOKEZA WATU WENGINE WATATU AMBAO KWA PAMOJA WALIMVAMIA, KUMJERUHI NA KISHA KUMPORA PIKIPIKI HIYO. 

AIDHA, KUTOKANA NA TUKIO HILO, MTUHUMIWA MMOJA AITWAYE NASIBU KIBONA [23] MKAZI WA MAJENGO AMEKAMATWA BAADA YA WENZAKE HAO WATATU KUKIMBIA NA PIKIPIKI HIYO. JUHUDI ZA KUWATAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA KITUO CHA AFYA TUNDUMA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUJITAFUTIA KIPATO KWA NJIA HALALI NA KUACHANA NA TAMAA YAN MALI KWA NJIA ZISIZO HALALI.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo