Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Agustino Lyatonga Mrema amesema kuwa kushindwa kwake ubunge kulitokana na michezo mchafu uliochezwa na mshindi wa ubunge wa jimbo hilo, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR-MAGEUZI, James Mbatia
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mrema amesema kuwa mshindi wa jimbo hilo amekuwa akionywa na msimamizi wa uchaguzi kutokana na matumizi ya vipeperushi ambavyo yeye alijipigia kura ya ubunge katika jimbo la Vunjo.
Mrema amesema matokeo ya yaliyompa ushindi Mbatia hakusaini kutokana na kufanya hujuma nyingi ikiwa ni pamoja na kumsema mgombea mwenzake.
Aidha amesema kuwa katika kipeperushi chake Mbatia sehemu ya bendera ya TLP yenye alama ya jogoo ilionekana kifaranga baada ya kuwa na jogoo mkubwa anayewika.
Mrema katika kukutana na waandishi pia alimpongeza Rais Mteule wa CCM, Dk.John Pombe Magufuli kwa kura za kishindo na kutaka kuwa yuko naye.
Amesema kumpigia kampeni Mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli kulitokana na kazi nzuri ya kupeleka barabara katika jimbo lake akiwa Waziri wa Ujenzi.
Mrema katika mkutano wake leo aliambatana na viongozi wa juu wa chama hicho kueleza hujuma alizofanyiwa katika uchaguzi katika jimbo la Vunjo akimhutumu, James Mbatia ambaye ameibuka kidedea katika uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP),Agustino Lyatonga Mrema akizungumza leo na waandishi habari juu ya kufanyiwa rafu katika jimbo la vunjo na kusababisha kushindwa kulitwa kwa mara nyingine kushoto ni aliyekuwa Mgombea Urais wa TLP ,Maxmillian Lyimo , na Kulia Katibu Mkuu wa TLP,Nancy Mricaria.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Agustino Lyatonga Mrema akionyesha moja ya kipeperushi kilichomsababisha kukosa jimbo hilo kushoto ni aliyekuwa Mgombea Urais wa TLP, Maxmillian Lyimo , na Kulia Katibu Mkuu wa TLP, Nancy Mricaria.
Mwenyekiti wa Umoja Wanawake wa Vunjo,Venancia Nicholaus akizungumza na waandishi juu ya wanawake wa vunjo walivyopata pigo kuungushwa kwa mgombea wao Mrema kwa hujuma za Mbatia kulia ni Mgombea Ubunge Bunda Mjini,Dk.Lucas Webiro leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Agustino Lyatonga Mrema leo jijini Dar es Salaaam.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii