Mbaroni kwa kuwafungia Watoto yatima na kuwaweka Kinyumba

MKAZI mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Joseph Bagule (61) mkazi wa Kilimahewa Kata ya Maili moja Mjini Kibaha Mkoani Pwani, anatuhumiwa kuwafungia watoto yatima ndani na kuwaweka kinyumba.
Taarifa zilizothibitishwa na Jeshi la Polisi mkoani humo zinaeleza kuwa, Joseph (61) anatuhumiwa kuwafungia wajukuu zake wawili akiwemo mwenye umri wa miaka (16) na Mtoto wa Dada yake mwenye miaka (25) ambapo amezaa nao watoto.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Jafari Ibrahim, amesema kwamba mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
Aidha, amesema mbali na kumshikilia mtuhumiwa, kwasasa wanafanya vipimo vya vinasaba (DNA) kwa ajili ya kupata uhakika kama ni kweli mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuzaa na wajukuu wake kuwa ni kweli au la!
Blog hii inaendelea kufuatilia tukio hilo kwa karibu na kadri itakavyopata taarifa zaidi itawajulisha wasomaji wake kile litakachojiri.
Chanzo: Fikra pevu


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo