Idara ya afya mkoani Kagera imekanusha kuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu mkoani humo baada ya taarifa za kupokelewa kwa wagonjwa kadhaa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera Thomas Rutachunzibwa amekiri kuwepo na wagonjwa kumi na wanne ambao hapo awali walikuwa na dalili za ugonjwa huo na kisha kuthibitika kutosumbuliwa na maradhi hayo baada ya kufanyiwa vipimo.
Maeneo ya biashara ya vyakula yanayojumuisha watu wengi kwa pamoja kama vile stendi na masoko ni moja ya maeneo ambayo tahadhari ya ugonjwa wa kipindupindu inabidi ichukuliwe kwa umakini mkubwa.
Mama lishe katika stendi kuu ya mjini Bukoba wanasema wao tayari wamechukua tahadhari kubwa kufuatia kuwepo kwa habari za ugonjwa wa kipindupindu mjini humo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera Thomas Rutachunzibwa anakanusha taarifa za hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kupokea wagonjwa wa kipindupindu .
Licha ya kuwepo kwa mgao wa maji katika baadhi ya maeneo,Mamlaka ya maji safi na maji taka ya Mkoa wa Kagera (BUWASA) imekanusha kuwa na miundombinu mibovu ya maji
Aidha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera Daktari Thomas Rutachunzibwa, ametoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu ikiwa ni pamoja na kuzingatia afya ya msingi kama vile kusafisha mazingira,kula chakula cha moto,kuchemsha maji ya kunywa na kunawa mikono kabla na baada ya kula .