Walinzi wa Bar wafanyiwa kitu mbaya Geita

Walinzi wawili wanaolinda katika baa ya Wacha Waseme na Lunguya mjini Geita wamejeruhiwa na vitu vyenye ncha kali ambavyo vimesababisha kifo cha mlinzi mmojawapo.
Mlinzi huyo aliyejulikana kwa jina moja la Michael amefariki dunia baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita.
Tukio hilo limejiri majira ya usiku wakati walinzi hao wakiwa wamelala katika lindo ambapo watu wasiojulikana wanadaiwa kuvamia na kuwashambulia na kuvinjwa katika baa ya lunguye na kuiba shilingi elfu tisini na nane.
 Majeruhi ambao walifikishwa katika Hospitali ya Geita majira ya asubui na kupewa matibabu ambapo mchana Michael alifariki dunia.
Wananchi wa Geita wamesema kuwa hili ni zaidi ya tukio la tano linalohusu walinzi kuuwawa na kuomba jeshi la Polisi kuhakikisha wanawakamata watuhumiwa waliohusika.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Peter Kakamba amethibitisha kutokea kwa Tukio hilo na msako unaendeshwa wa kuwakamata waliohusika.
 Majeruhi mmoja aliyejulikana kwa jina la Musa Buberwa bado anaendelea na matibabu Hospitalini hapa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo