Ruvuma waahidi kumuunga mkono Rais Magufuli

Wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wamesema wanaungana na Rais John Magufuli katika kuijenga Nchi kimaendeleo na kiuchumi.
Wakazi hao wamemuomba Rais Magufuli kuzipa kipaumbele changamoto zinazoukabili Mkoa wa Ruvuma kama viwanda, pembejeo za kilimo na kukuza mitaji.
Wananchi hao wamesema katika Vitabu vya Dini vinasema Roho ya Mungu ilitulia katika Maji, na Dalili ya Mvua iliyonyesha wakati anaapishwa Rais Mteule Dr John Pombe Magufuli  ni ishara ya kuonyesha mkono wa Mwenyezi Mungu upo pamoja na Rais Mteule wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania
 Wananchi  wamemwomba Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania kusafisha mabaya yote ambayo yalikuwa nalenga chama cha CCM Pamoja na kutelkeleza ahadi alizo ahidi na kuunda baraza la mawazizili lenye mtazamo wake na siyo vinginevyo
            Vijana nao wamesema Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr. John Pombe Magufuli alihaidi Mikopo kwa Vijana pia kuboresha Maisha ya Watanzania na ahadi zake amehaidi kwa kumtanguliza  Mwenyezi Mungu.       
Wazee wa Mkoa wa Ruvuma wakiongozwa na Mkurugenzi wa Shirika la PADI Iskaka Msigwa wamesema Kiongozi Bora utamjua kutokana na kauli zake. Hotuba fupi aliyoitoa Mheshimiwa Rais Mteule Dr. John Pombe Magufuli imeonyesha haina ubaguzi  kwa mtu yeyote inawakusanya  wa Tanzania wote.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo