Aua wake zake kwa jembe

Watu sita wamefariki dunia Mkoani Singida  katika matukio manne tofauti likiwemo tukio la wanawake wawili kuuawa kikatili kwa kukatakatwa kwa jembe sehemu mbalimbali za miili yao na mume wao.
Kamanda wa Polisi Singida Thobias Sedoyeka aliwataja wanawake hao mbele ya waandishi wa habari kuwa ni Mwanahamisi Juma na Mwanahamisi Abrahani wote wakazi wa kata ya Mgori, Singida.
Alisema Mustapha Said ambaye alikuwa mume halali wa mwanahamis Juma anatuhumiwa kuhusika na mauaji hayo na alitekeleza unyama huo baada ya kuwakuta wanawake hao wakilifanyia usafi shamba lao kwa ajili ya kupanda mbegu.
Kamanda Sedoyeka alisema mwanaume huyo naye aliuawa na wananchi waliokuwa wamejaa hasira kali.
Chanzo cha mauaji hayo inasemekana mwanaume huyo huyu alikua ametalikiana na mke wake wake wa kwanza na walikua katika ugomvi wa shamba lao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo